Skip to main content

Nuh Mziwanda - Anameremeta Lyrics

Wanasema sare sare maua tunafanana
Shida zetu wenyewe tunazijua tunaendana
Mwenzangu kamoyo kangu kadogo kukuru kakara kanashindwa
Hakuna manati bila kipago bila ya wewe nitashindwa
Macho yangu ninafumba sitamani mwingine
Na penzi langu sio tunda akang’ata mwingine
Hado hado tunajikongoja tutafika domo macho ukaribu wetu kama mapacha hado hado
Tunajikongoja tutafika domo macho ukaribu wetu kama macha
Anameremeta anameremeta
Kasura kake kazuri anameremeta
Mcheshi hana kiburi anameremeta
Kanipa mtoto naringa anameremeta
Tumbo joto amevimba anameremeta
Suti na shera kama masihara harusi imefika
Sina papara ubachelor jiko nimevuta
Kiziwi kweli hasikii na kipofu haonii
Mi kuwa kwako sijutii utamu kisogoni
Litunze penzi langu mama maradhi ni mengi wee
Maji kupwaa nisije kuzama penzi sio vazi liazimwee
Hado hado tunajikongoja tutafika domo macho ukaribu wetu kama mapacha hado hado
Tunajikongoja tutafika domo macho ukaribu wetu kama macha
Anameremeta anameremeta
Kasura kake kazuri anameremeta
Mcheshi hana kiburi anameremeta
Kanipa mtoto naringa anameremeta
Tumbo joto amevimba anameremeta
Anameremeta kasura kake kazuri
Mcheshi hana kiburi
Kanipa mtoto naringa (naringa)

Popular posts from this blog

Diamond Platnumz - Sikomi (Translation in English) Lyrics

Verse 1 Wanasemaga mapenzi safari,  Unavyopita ndo jinsi unajongea They say love is a journey, the more you move the closer you get (to real love) Ila niendako ni mbali sijui ka ntafika sababu natembea But it seems I'm going far, and I'm not sure I'll reach since I'm walking . Niliposikiaga Habari,  Yakisifika nikakesha nangojea I heard the news of praises (when starting off as a musician) I stayed up at night waiting Akabariki Jalali na nikawika muziki nikauotea God poured his blessings and I delved into music,  Ile pruuu mpaka Macca,  Nikadandiaga Bongo movie,  Kumbe mapenzi hayataki haraka While still in my pilgrimage (not yet 'arrived' as a musician), I hoped on to (fell in love with) a 'movie artist'  I still didn't know "love is slow"/love requires patience, there's no need to rush Ni kama tango natia tu chumyi I was impatient adding salt, eating a fruit when it wasn't yet ripe (Okay the word tango means a fr...

Beka - Natumaini Lyrics

Ni upendo, natamani nikuone japo sura iniponye… We ndio nyota yangu kama TID Nikuudhi usinikimbie kama Amini Natumaini utanielewa zaidi ya yule Beka Nikuudhi ntakubembeleza kama Barnaba boy Usininywishe sumu ya mapenzi, Usiwe mama mbaya Mimi sio mgeni wa mapenzi, mwaumivu nayajua Sio kisa pombe pombe ulonifanya niropoke Sio kisa pombe pombe ulonifanya niropoke Ooh daima na milele mi nitakuwa nawe Maisha yangu yote kama Marlaw Daima na milele eeh mimi nitakuwa nawe, maisha yangu yote aah Hutosema bora ukimbie, kama Lina ooh Usiende kwa mganga kama Kasimu ooh

Christina Shusho - Ee Bwana Umenichunguza Lyrics

Ee bwana umenichunguza, nakunijua Wewe wajua kuketi kwangu, na kuondoka kwangu Umelifahamu wazo langu, tokea mbali Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu Umeelewa na njia zangu zoote Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu Umeelewa na njia zangu zoote