Wewe wajua kuketi kwangu, na kuondoka kwangu
Umelifahamu wazo langu, tokea mbali
Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu
Umeelewa na njia zangu zoote
Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu
Aaah uuuh mmmh
Maana hamna neno uilmini mwangu, usilojua kabisa Bwana
Umenizingira nyuma na mbele, ukaniwekea mkono wako
Maarifa haya ni ya ajabu, yanishinda mimi, hayadhihiriki
Siwezi kuyafikia, hayadhihiriki, Siwezi kuyafikia
Niende wapi nijiepushe, na Roho yako
Niende wapi niukimbie uso wako
Kama ningepanda mbinguni wewe uko
Ningefanya kuzimu kitanda, huko nako uko
Kama nikisema hakika giza litanifunika,
Giza nalo halikufichi kitu,
Giza na mwanga kwako ni sawasawa
Ee Mungu unichunguze, ujue moyo wangu
Ee Mungu (Ee Mungu eee)
Unijaribu, uyajuwe mawazo yangu
Eeh Mungu (Ee Mungu)
Eeh Mungu (Uone kama)
Uone kama niko njia iletayo majuto ndani yangu
(Eeh Mungu ee) Eeh Mungu (Ukaniongoze)
Ukaniongoze katika njia ya haki (mileeele) milele
(maana wewe)
Maana wewe ndiwe uliye niumba (uzima wangu)
Uzima wangu (Eeh Mungu ee) Ee Mungu
(Macho yako)
Macho yako yaliniona kabla sijakamilika (eeh Mungu ee) Ee
Mungu
(Nimekuita)
Uisikie sauti yangu (Nikuitapo baba)
Eeh Mungu (Eeh Mungu Ee)
Ee Mungu (Ee Mungu)
Ee Mungu unichunguze, ujue moyo wangu
Ee Mungu (Ee Mungu eee)
Unijaribu, uyajuwe mawazo yangu
Eeh Mungu (Ee Mungu)
Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo
Yapate kibali mbele zako
Eeh Mungu (Ee Mungu)
Eeh Mungu
Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo
Yapate kibali mbele zako
Eeh Mungu
Eeh Mungu
Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo
Yapate kibali mbele zako
Oooh ooh
Eeh Mungu, Eeh Mungu